Simba imeukaribisha vyema msimu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamo kwenye mchezo wa kilele cha Sportpesa Simba Week
Mashabiki waliujaza uwanja wa Taifa kuwaona wachezaji wao wapya, hakika wameburudika
Ingawa bado ni mapema, lakini kwa kilichoonyeshwa na mnyama leo, Wana Msimbazi wana uhakika wa kuwa na msimu mwingine wa furaha
Wachezaji wote wapya wamecheza vizuri lakini winga Deo Kanda na viungo Francis Kahata na Sharaff Shiboub waliipendezesha zaidi Simba

Mashabiki wengi wameridhishwa na kiwango cha Simba leo, bila shaka huu ni mwanzo tu
Meddie Kagere 'MK14' ameendeleza pale alipoishia msimu uliopita, pengine msimu huu anaweza akaweka rekodi ya kupachika mabao kwani amezunguukwa na mafundi wa mpira ambao watakuwa wakimrahisishia kazi
Katika mchezo huo Simba haikuwa na nyota wake saba ambao juzi waliitumikia timu ya Taifa nchini Kenya
Aussems aliwapa mapumziko wachezaji hao ili wawe tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo ambao utapigwa Jumamosi nchini Msumbiji