Michango yamkatisha tamaa Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2019
Michango yamkatisha tamaa Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hataendelea kubaki katika klabu hiyo kama Wana Yanga hawatajitoa kuichangia timu kwa ajili ya mipango ya msimu ujao

Akihojiwa na moja ya redio maarufu nchini, Zahera amesema amekuwa akijitoa kuisaidia Yanga na alitarajia Wana Yanga nao watafanya hivyo wakati huu ambao timu inapita katika kipindi kigumu lakini hali imekuwa tofauti

"Wanasema Yanga ni timu ya Wananchi lakini mbona wananchi hao hawaonekani kuisaidia timu?" alihoji Zahera

"Msimu huu hatukuwa na malengo ya kutwaa ubingwa, sababu iko wazi, kikosi chetu hakijakamilisha mahitaji ya kuweza kuwa mabingwa"

"Nilitegemea Wana Yanga watachangia timu kama tulivyopendekeza ili msimu ujao tuweze kuwa na kikosi imara zaidi"

"Lakini kwa hali inavyoendelea mimi sitakuwa tayari kufanya kazi kwenye timu ambayo haina malengo."

"Sitakuwa tayari kuendelea kuwasaidia watu ambao wenyewe hawajisaidii"

Zahera amefanya kazi kubwa msimu huu ambapo licha ya mapungufu yaliyopo, ameweza kuiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikipoteza michezo miwili tu

Kocha huyo Mcongomani anataka kuiona Yanga inatoka katika 'ukata'.

Pendekezo la kuwataka Wana Yanga waichangie timu yao ni moja ya njia za muda mfupi zinazoweza kuifanya Yanga ikasimama wakati ikiendelea kuandaa mikakati ya kuweza kujitegemea kama walivyo watani zao Simba

Hata hivyo muitikio mdogo wa Wana Yanga katika kutoa michango umemfanya kocha huyo akate tamaa na pengine huenda akaondoka mwishoni mwa msimu kama mambo hayatabadilika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’