Waziri Mkuu kuongoza shamrashamra za Simba Day

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Aug 2019
Waziri Mkuu kuongoza shamrashamra za Simba Day

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kesho katika kilele cha Sportpesa Simba Week

Akizungumza leo kwenye uwekaji jiwe la Msingi uwanja wa Simba Bunju, Mo amesema kesho ni siku muhimu kwa Wanasimba kuonyesha ukubwa wa klabu yao

Aidha Mo amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ataungana na Wanamsimbazi katika tukio hilo la kihistoria

"Nawaambia Wanasimba wote, kesho ndio kesho, tukaujaze uwanja wa Taifa ili kuwaonyesha Watanzania ukubwa wa klabu yetu," amesema

"Waziri Mkuu wetu Mh Majaliwa Kassim Majaliwa ataungana nasi katika sikukuu yetu rasmi"

Katika hatua nyingine, Mo amesema kuwa wamekubaliana na Bodi ya klabu hiyo kuwa kutakuwa na Gala itakayohudhuriwa na mashabiki zaidi ya 500 kwa ajili ya kuchangia hasa katika uboreshaji wa viwanja vilivyozinduliwa leo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’