Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikabili Alliance Fc katika mchezo wa ligi
Kikosi cha Yanga kiko Mwanza tangu juzi kikijiandaa na mchezo huo ambao mabingwa hao wa kihistoria wamepania kuchukua alama zote tatu
Kocha Mwinyi Zahera amesema ana matumaini makubwa kwa vijana wake kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo kutokana na maandalizi waliyofanya
Yanga leo itawakosa wachezaji kadhaa akiwemo beki Andrew Vicent ambaye anasumbuliwa na maumivu ya misuli
Pamoja na mchezo wa Yanga, michezo mingine mitatu inatarajiwa kupigwe leo katika viwanja mbalimbali
JKT Tanzania vs Coastal Union
KMC vs Biashara United
Ruvu Shooting vs Mwadui FC
ADVERTISE HERE