Aliyekuwa beki wa kushoto wa Simba Asante Kwasi yuko katika hatua za mwisho kujiunga na Baroka Fc inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Kwasi anaondoka Simba baada ya uongozi wa timu hiyo kuamua kuachana nae
Katika klabu ya Baroka Fc ataungana na beki wa zamani wa Simba Abdi banda ambaye alijiunga na timu hiyo msimu uliopita
Licha ya mkataba wake kumalizika mwezi ujao, uongozi wa Simba tayari umemkabidhi barua ya kumtaarifu kuwa hawataendelea nae baada ya mkataba wake kumalizika
Nafasi yake imechukuliwa na Gadiel Michael aliyesajiliwa kutoka klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE