Baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Simba, Yanga inaelekea mkoani Mwanza kuikabili Mbao Fc katika mchezo utakaopigwa Jumatano, Februari 20 kwenye dimba la CCM Kirumba
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Mwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wamesahau matokeo ya mchezo wa jana na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo dhidi ya Mbao Fc
Yanga itakuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Mbao Fc katika dimba la CCM Kirumba
Yanga haijawahi kuondoka na pointi katika dimba la CCM Kirumba katika michezo iliyocheza na Mbao tangu timu hiyo ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita
Katika hatua nyingine uongozi wa Yanga umewashukuru wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano waliotoa kuelekea mchezo dhidi ya Simba
Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amesema licha ya kupoteza mchezo wa jana, hawajapoteza malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu
Amewataka Wana Yanga waendelee kuwa wamoja na wasiache kuichangia timu yao ili iweze kutimiza malengo yake
Baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc, Februari 24 Yanga itachuana na Namungo Fc katika mchezo wa raundi ya tano, kombe la FA (ASFC), mchezo utakaopigwa dimba la Majaliwa wilayani Ruangwa