Aliyekuwa mlinda lango wa Simba Said Mohammed 'Nduda' amesajiliwa na Mtibwa Sugar, timu aliyowahi kuichezea kwa nyakati tofauti
Nduda ambaye msimu uliopita Simba ilimtoa kwa mkopo kunako klabu ya Ndanda Fc, ametua Mtiwa Sugar baada ya mkataba wake kumalizika
Mlinda lango huyo aliyetua Simba baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya COSAFA iliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2017, alipoteza nafasi kwenye kikosi cha Simba mwaka jana baada ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kumsajili Deogratius Munishi 'Dida'
Hata hiyo Dida nae ameondoka baada ya usajili wa Beno Kakolanya aliyetokea Yanga
Msimu huu walinda lango watatu wa Simba ni Aishi Manula, Beno na Ally Salim
ADVERTISE HERE