Bado wapo baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao wameendelea 'kumlilia' Beno Kakolanya arudishwe kikosini kuelekea mchezo ujao dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, Februari 16 katika uwanja wa Taifa
Baadhi yao wasichofahamu ni kuwa Beno mwenyewe ndiye aliyeomba kuvunja mkataba wake na Yanga.
Mpaka sasa uongozi wa Yanga uko katika majadiliano na Mwanasheria wake ili waweze kumruhusu aendelee na maisha yake
Hivyo haitawezekana kwa Yanga kumrudisha Beno ili adake mchezo dhidi ya Simba.
Na hata kama Yanga ikimrudisha Beno leo, ikumbukwe hajacheza mchezo wowote wa ushindani kwa zaidi ya miezi mitatu hivyo hawezi kuwa na 'utimamu' wa kutosha kumfanya aaminiwe kukaae langoni kwenye mchezo huo muhimu
Lakini pia kutomuamini Ramadhani Kabwili ni kutomtendea haki mlinda lango huyo mdogo zaidi katika ligi kuu ya Tanzania Bara
Kabwili akisaidiana na Klaus Kindoki ndio waliodaka michezo mingi kuliko Beno. Kwa maana hiyo mafanikio ya Yanga kuwa kileleni katika msimamo wa ligi yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na wao
Beno alifanya vizuri katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, alitimiza wajibu wake lakini haimaanishi makipa wengine waliopo Yanga hawawezi kufanya vizuri wakipewa nafasi
Baada ya kuwa amepona kabisa majeraha ya nyonga yaliyokuwa yakimsumbua, Kabwili ameonyesha kuimarika zaidi.
Katika mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania, Kabwili alifanya kazi kubwa na alidhihirisha kinda huyo amekomaa
Kabwili ni miongoni mwa walinda lango wenye vipaji sana hapa Tanzania. Licha ya umri wake mdogo, Kabwili tayari ameshiriki katika michezo mikubwa yenye presha na ushindaniΒ mkali
Kabwili alihitaji nafasi kama hii ili aongeze uzoefu na kujiamini. Wana Jangwani hawana sababu ya kuwa na hofu anapokuwa langoni