Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imesema haina taarifa za Mzee Hamisi Kilomoni kuwa mdhamini wa klabu ya Simba
Rita imesema kuwa hakuna rekodi inayoonyesha Kilomoni kama bado yupo kwenye nafasi hiyo kwa sasa.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Rita, Josephat Kimaro amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akisema taarifa walizonazo Rita zinawatambua wadhamini wanne lakini Kilomoni si miongoni mwao.
"Rekodi zetu tangu Novemba 2017 zinaonyesha wadhamini wa Simba ni Ramesh Patel, Abdul Abbas, Idd Mgoyi na Profesa Juma Kapuya," alisema Kimaro.
Alipoulizwa taratibu ambazo zinafanyika hadi mdhamini kuondolewa, Kimaro alisema zimewekwa kwenye mtandao wa Rita ambao ni www.rita.go.tz.
Katika mtandao kipengele cha mabadiliko ya chombo, jina au marekebisho ya mdhamini kinasema lazima kuwalisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu ya mkutano uliothibitishwa ambao ulifanya mabadiliko ya jina na kurejesha cheti halisi cha zamani.
Kifungu kingine kinaeleza Hairuhusiwi kumiliki ardhi au haki kwenye ardhi, bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa wadhamini (Kabidhi Wasii Mkuu). Kumtaarifu Msimamizi Mkuu wa wadhamini juu ya mabadiliko yoyote, mabadiliko ya wadhamini, jina la chombo, anwani ya posta, Katiba ndani ya mwezi mmoja.
Akizungumzia barua iliyoonyeshwa juzi Jumanne na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, Kimaro alisema ni barua halali kutoka Rita.
βNi kweli ile ni barua yetu na kwenye kumbukumbu zetu huku Rita Patel, Abbas, Kapuya na Mgoyi ndiyo wadhamini wa Simba, kwa wengine sifahamu kumbukumbu za nyuma zilikuwa vipi, ila kuanzia Novemba 2017 hao ndiyo wanasomeka kwetu,β alisema Kimaro.
Kimaro alisema tangu Novemba 2017 Rita haijapata malalamiko yoyote ya mtu au watu kupinga kuhusu mabadiliko hayo ya wadhamini.