Simba yasajili wachezaji 26

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jul 2019
Simba yasajili wachezaji 26

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori amesema timu hiyo imekamilisha usajili wa wachezjai wa kikosi cha kwanza kwa asilimia 99 ikiwa imesajili wachezaji 26

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Magori amesema bado hawajakamilisha usajili wa mchezaji mmoja tu

"Tumesajili jumla ya wachezaji 26, kikosi Cha kwanza, wachezaji wameelekea Afrika Kusini na wengine wakikamilisha pasi zao basi na wao watasafiri kuwafata wenzao," amesema

"Lakini katika usajili unaweza kusema kama usajili umekamilika ingawa imebaki nafasi moja lakini niwaombe mashabiki wavute subra"

Magori amesema pia Simba itasajili wachezaji wa kikosi cha timu ya vijana pamoja na timu ya Wanawake, Simba Queens

Aidha Magori amesema Simba itacheza michezo mitatu ya kirafiki huko Afrika Kusini ilikoweka kambi

Mchezo wa kwanza utapigwa Julai 23 2019

"Timu ipo kambini na inaendelea na mazoezi lakini kwenye program yetu tunarajia kucheza Michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kurejea Nyumbani na mchezo wetu wa kwanza tutacheza Tarehee 23/7/2019"

Katika hatua nyingine, Magori amesema Simba itakuwa na jezi za aina tatu tofauti ili kukidhi matakwa ya mashindano ambayo timu hiyo itashiriki

"Tukija kwenye upande wa jezi, Simba tunataka tuwe na jezi tatu kutokana na matakwa ya Caf, Jezi nyekundu Nyumbani, jezi jeupe na Kijivu zenyewe zitakuwa zikitumika ugenini"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’