Usajili wa beki Gerson Fraga Vieira umekamilisha safu ya ulinzi ya Simba ambayo sasa ina watu wa kazi
Fraga raia wa Brazil ametambulishwa leo na uongozi wa Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili
Beki huyo sasa anakamilisha ukuta wa Simba ambao sasa utaundwa na watu wa kazi wakiongozwa na Paschal Wawa, Erasto Nyoni, Yusufu Mlipili, Kenedy Juma, Paul Bukaba na Sharif Shiboub ambaye ni kiraka anayemudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji na beki





Ukuta huu utakuwa na jukumu la kuibeba Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Moja ya changamoto iliyoikabili Simba msimu uliopita kwenye michuano hiyo ni safu ya ulinzi, ambapo kipaumbele kikubwa msimu huu ilikuwa kuboresha eneo hilo
Simba imesajili wachezaji wapya watatu eneo la ulinzi/kiungo wa ukabaji wawili wakiwa na kigeni na mmoja mzawa