Kesi ya Wanachama Yanga yapigwa kalenda hadi Januari 24

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
14 Jan 2019
Kesi ya Wanachama Yanga yapigwa kalenda hadi Januari 24

Kesi iliyofunguliwa na Wanachama wa Yanga jijini Dar es salaam kupinga uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizowazi uliokuwa ufanyike jana, Januari 13 2019, itatajwa Januari 24 2019.

Wanachama wa klabu ya Yanga, Juma A. Magoma na Athuman S. Nyumba walifungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1/ 2019  kupinga kufanyika kwa uchaguzi wa kuzaja nafasi zilizoachwa ndani ya Kabla ya Yanga.

Magoma na Nyumba walifungua shauri hilo Januari 11, 2019 na kupangwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.

Katika madai yao wakipinga kufanyika kwa uchaguzi huo kwa madai ya unakwenda kinyume na katiba ya Klabu ya Yanga ya mwaka 2010 ibara ya 7.

Ibara hiyo inaelezea utaratibu wa uanachama ndani ya Klabu ya Yanga ambao, kwanza ni kutuma maombi, ambapo maombi hayo yatapelekwa kwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, ambaye baaade yatajadiliwa na kamati tendaji.

Pia, ibara hiyo, inaelezea kuwa maombi hayo yataambatana na fomu namba YASC/U, ada ya uanachama ambayo ni Sh 12,000 pamoja ana ada ya kadi ambayo ni Sh 2000.

Pia wanadai kuwa kuna taarifa za kuwepo kwa wanachama wenye kadi feki za kieletroniki ambazo zinasaini na mhuri ambazo zinasambaa kwa baadhi ya wanachama, ambazo zinaonyesha kuwa zimetolewa na benki ya CRDB pamoja na benki ya Posta, zinazodaiwa kuwa ni kadi za uanachama wa Klabu ya Yanga, zikiwa na picha za wamiliki ambazo sio mali ya klabu hiyo.

Kwa makusudi yoyote, kadi hizo za kielektroniki  zilizotolewa na CRDB na benki ya Posta, kwa namna yoyote ile haziwezi kuwa uthibitisho wa uanachama wa Yanga, kupitia kwa kuzingatia kwamba , wahusika wa hizo kadi, hawakupitia utaratibu ulioanishwa katika ibara ya 7 ya mwaka 2010 ya klabu ya Yanga.

Wanachama hao wanadai pia, kumpa mtu anachama bila kadi hiyo kusainiwa na kukong’wa muhuri wa klabu, haiwezi kutumika kuanisha uanachama wenye haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa klabu ya Yanga.

Wanadai kuwa utaratibu wa kazi za uanachama zilizotolewa na benki hizo, mpaka sasa haufahamiki wala hauna uthibitisho katika katiba ya Yanga.

Hata hivyo, ikiwa maombo hayo hayatakubaliwa watapata hasara ambayo haiwezi kufidiwa sababu kwa kuwa na matokeo ya uchaguzi ambayo hayaakisi maslahi ya wanachama na kupata viongozi ambao hawana Baraka kutoka klabu ya Yanga.

Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, 2019, itakapotajwa.

CC : Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →