Kennedy awataka mashabiki watulie, wasubiri 'mavitu' yake dimbani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jun 2019
Kennedy awataka mashabiki watulie, wasubiri 'mavitu' yake dimbani

Beki Kennedy Juma aliyetua Simba kutoka klabu ya Singida United amewataka mashabiki wa timu hiyo kutulia, wasubiri kazi yake uwanjani

Usajili wa Kennedy ambao ulipendekezwa na kocha Patrick Aussems, ulipokewa tofauti na baadhi ya mashabiki wa Simba ambao wanaamini timu hiyo ilihitaji beki imara zaidi atakayeisaidia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa

Hata hivyo Kennedy aliyeitumikia Simba kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Gwambina Fc jana, anaamini mashabiki hao wataikubali kazi yake

"Kikubwa ni kumuomba Mungu atujalie afya, nina amini watashangaa, nitapambania namba kwa sababu ushindani najua utakuwa mkali kwahiyo wasubiri tukutane uwanjani”

Beki huyo aliongeza kuwa kujiunga na mabingwa hao ni kama njia ya kujitangaza zaidi kwani timu yake inashiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Alisema moja ya mkakati wake ni kuhakikisha anatumia vyema nafasi atakayopata chini ya Kocha Patrick Ausesms ili kufikia malengo ya kazi yake hiyo.

"Mashabiki wategemee vitu vizuri, Simba ni timu kubwa inayojiandaa na michuano ya kimataifa kwahiyo lazima nitumie nafasi hiyo kuonyesha uwezo mkubwa kufikia malengo yangu"

Simba imemsajili Kennedy kuimarisha safu yake ya ulinzi. Inaelezwa mabingwa hao wa Tanzania Bara watasajili beki mwingine wa kigeni ambaye ataungana na Kennedy pamoja na walinzi waliopo kuunda ukuta mpya wa Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’