Beki kisiki anayetajwa kusubiri utambulisho Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jun 2019
Beki kisiki anayetajwa kusubiri utambulisho Simba

Uongozi wa Simba umemalizana na nyota wawili wa kigeni ambao inaelezwa wako jijini Dar es salaam kukamilisha taratibu za usajili

Nyota hao mmoja ni raia wa Brazil na mwingine wa raia wa Sudan ambaye anacheza nafasi ya kiungo

Beki wa Brazil

Jina lake ni Gerson Viera, beki kisiki mwenye umri wa miaka 26 ambaye alizaliwa Porto Alagre huko Brazil.

Huyu ndiye hasa ambaye uongozi wa Simba ulimuweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii jana saa saba mchana ambaye sura yake ilileta mkanganyiko na yule mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Ryan Moon ambaye wasifu wake hauendani kusajiliwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara

Viera alikuwa akicheza klabu ya Atletico de Kolkata ya India akiisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa nchini humo mara mbili

Kabla ya kuondoka Brazil kusaka maisha kwingine, Viera aliichezea kwa mafanikio klabu maarufu ya Gremio ambayo ilitoa nyota kama Neymar, Coutinho, Casemiro na wengine kibao

Ni mchezaji aliyepata mafanikio makubwa sana ligi kuu ya India na bila shaka kitengo cha kusaka wachezaji cha klabu ya Simba (scouting) kimefanya kazi yake vizuri kum-baini mchezaji huyu kutoka nje ya bara la Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’