Dk Tiboroha azindua Kampeni Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2019
Dk Tiboroha azindua Kampeni Jangwani

Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Jonas Tiboroha alipitishwa kwenye mchakato wa kwanza wa kujaza nafasi zilizowazi na anaendelea na mchakato wa uchaguzi utakaofanyika Jumapili.

Alizindua kampeni Januari 09 2019 Makao Makuu ya klabu ya Yanga Jangwani, jijini Dar es salaam.

Dk Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga alitaja baadhi ya vipaumbele vyake kuwa kuwa ni; Kuirudisha klabu kwa Wanachama, Kujenga na kusimamisha Taasisi, Uwekezaji na Biashara, Kuimarisha Matawi na Kuimarisha mifumo ya uwendeshaji wa timu.

Kuhusu mabadiliko Dk Tiboroha amesema atashirikiana na Wanachama wa Yanga kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa kukaribisha wawekezaji huku Wanachama wakiendelea kubaki wamiliki wakuu wa klabu hiyo.

Chini ya Uongozi wake Dk Tiboroha amesema atabuni mipango ya maendeleo kwa kushirikiana na Wanachama wa Yanga kuhakikisha timu hiyo inanufaika kupitia uwekezaji mdogo na mkubwa.

"Chini ya uongozi wangu nakusudia kurudisha klabu kwa wanachama," amesema

"Tuna maana ya kuwa pamoja na kupanga kuhamia kwenye mfumo wa kisasa kwa maana ya kutoa nafasi kwa wawekezaji lakini wanachama watabaki kama wamiliki wakuu wa klabu, hili tumelifanyia uchunguzi makini"

Dk Tiboroha ambaye kitaaluma ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ana uzoefu wa uongozi katika klabu ya Yanga kwani amewahi kuhudumu nafasi ya Katibu Mkuu kabla ya kujiuzulu Januari 2016 kutokana na sababu binafsi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’