Wakala wa mchezaji Juma Balinya ambaye juzi alisajiliwa na Yanga, Patrick Gakumba amesema alimpeleka Yanga mshambuliaji huyo kutoka Uganda baada ya klabu ya Simba kumkataa
Balinya alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu ambao waliletwa na Gakumba ili wasajiliwe na Simba
Hata hivyo amesema kutokana na aina ya washambuliaji ambao tayari Simba wanao, walipendekeze awaletee mshambuliaji mwenye rekodi kubwa barani Afrika ambaye ataweza kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hasa kuvuka mafanikio waliyopata msimu uliopita
"Simba tayari ina washambuliaji ambao wanarekodi kubwa barani hivyo walihitaji mshambuliaji mwenye rekodi zaidi ya hawa waliopo," amesema
Balinya ni mshambuliaji mzuri, aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda msimu uliomalizika lakini hakufikia vigezo vilivyowekwa na Simba kwa mchezaji wanayemtaka"