Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori mapema leo alitolea ufafanuzi wa mkanganyiko wa usajili wa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo John Bocco ambaye anadaiwa kusaini mkataba wa kuitumikia Polokwane City inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Magori amesema Simba ilifahamu kuwa Bocco alisaini mkataba wa awali klabu ya Polokwane lakini mkataba huo sio rasmi na timu hiyo isingeweza kumsajili bila ya kuwasiliana na uongozi wa Simba
Amesema Simba ilimpa Bocco mkataba baada ya kujiridhisha kuwa mkataba aliosaini Polokwane City ulikuwa wa awali
"Polokwane walikosea kwa sababu hawakufuata taratibu, walijua Bocco ni mchezaji wetu, lakini wao naona walikuwa wanataka kama ushindani na sisi, hata huyo wakala sisi tulimuambia kabisa kwamba tayari tumemalizana"
"Mkataba wa awali unakua unamuonyesha mchezaji uhakika wa yeye kuhitajika, hao Polokwane wamempa Bocco mkataba juu ya mkataba kitu ambacho wamekosea na kama PSL wamepokea mkataba basi Fifa itahusika," amesema
cutUongozi wa Simba umetoa taarifa rasmi kuwatoa wasiwasi mashabiki na wanachama wake juu ya usajili wa Bocco, kwani ataendelea kubaki Msimbazi kwa miaka mingine miwili
Bocco yuko Misri ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 zinazoanza Juni 21