Ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Yanga leo dhidi ya Mbeya City umehakikishia timu hiyo kumaliza mwaka 2018 bila kupoteza mchezo katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu wa 2018/19.
Ushindi huo pia umeihakikishia Yanga kumaliza kileleni mwa msimamo wa ligi katika mzunguuko wa kwanza.
Aidha Yanga pia imeandika rekodi mpya kwa soka la Tanzania baada ya kufikisha alama 50 ikiwa imeshuka dimbani mara 18.
Heritier Makambo wa Yanga ndio aneyeongoza kwa mabao kwenye ligi akiwa amefunga mabao 11. Lakini pia Ibrahim Ajib anaongoza kwa kutoa pasi za mabao akiwa ameisadia Yanga katika mabao 13 huku pia akifanikiwa kufunga mabao matano.
Yanga ndio timu ambayo ina idadi kubwa ya wachezaji ambao wamefunga mabao.
Orodha ya wafungaji wa mabao ya Yanga
1. Heritier Makambo 11
2. Ibrahim Ajib 5
3. Amisi Tambwe 5
4. Mrisho Ngasa 4
5. Deus Kaseke 1
6. Vincent Andrew 1
7. Rafael Daudi 2
8. Kelvin Yondani 1
9. Feisal Salum 2
10. Jafary Mohammed 1
11. Abdalah Shaibu 2
Takwimu hizi ni lazima ziwatishe wale wanaochuana na Yanga katika mbio za ubingwa. Yanga hii ya Zahera sio ya kawaida!