Aussems ataja sababu ya kubadili kikosi kizima mchezo dhidi ya Sevilla

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 May 2019
Aussems ataja sababu ya kubadili kikosi kizima mchezo dhidi ya Sevilla

Jana Simba nusura iondoke na ushindi wa kihistoria dhidi ya Sevilla katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa ukimalizika kwa Sevilla kushinda mabao 5-4

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko ya wachezaji tisa kwenye kipindi cha pili, mabadiliko yanayotajwa kupunguza kasi ya Simba na kupoteza uongozi wa mchezo huo baada ya kuruhusu mabao matatu ndani ya dakika 10

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems ametetea uamuzi wake akisema ilikuwa muhimu kwa kila mchezaji kupata nafasi kwani ulikuwa ni mchezo wa kihistoria kwa wachezaji wa Simba

"Nilitaka kila mchezaji acheze dhidi ya timu bora kama ya Sevilla," Aussems aliwaambia waandishi wa habari

"Niliona ni fursa ya kila mchezaji kuweza kucheza mchezo huu dhidi ya Sevilla ili kuweza kupata Uzoefu zaidi ndio maana niliwapa nafasi wachezaji karibia wote kucheza mechi hii kubwa na ya kihistoria dhid ya klabu bingwa mara tano ligi ya Europa"

Simba iliongoza mchezo huo kwa muda mrefu lakini ikapoteza mchezo mwishoni

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco (2) aliyeibuka nyota wa mchezo, Meddie Kagere na Clatous Chama

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
30m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’