FT : Simba 2-0 Ndanda FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 May 2019
FT : Simba 2-0 Ndanda FC

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wanahesabu siku za kukabidhiwa ubingwa wa pili mfululizo baada ya leo kuichapa Ndanda Fc mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru

Wakicheza kandanda la pasi fupifupi lililojaa ufundi wa hapa na pale, Simba ilijipatia mabao yake yote mawili kwenye kipindi cha kwanza yote yakiwekwa kambani na Meddie Kagere 'MK14'

Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe alama 88 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 83

Yanga imebaki na michezo miwili, inahitaji kushinda yote ili kuweza kuipiku Simba lakini wakati huohuo Simba bado ina michezo mitatu mkononi

Ni muujiza pekee ambao utaifanya Simba isiweze kutwaa ubingwa!

Aidha Simba inaweza kwenda kumaliza 'shughuli' mkoani Singida keshokutwa itakapoivaa Singida United

cut

Kwenye mchezo huo Simba inahitaji alama moja tu kuweza kurejea na ubingwa jijini Dar es salaam

Kinara wa mabao Meddei Kagere amezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu baada ya leo kufikisha mabao 22

Kagere anaongoza kwa tofauti ya mabao sita dhidi ya Heritier Makambo na SalimAiyee ambao wote wana mabao 16

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’