Wakati leo Watanzania wakiadhimisha kumbukumbu ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Yanga itashuka uwanja wa Taifa kuikabili Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa moja usiku.
Yanga inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 38, ushindi utairejesha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo
Kikosi hicho cha kocha Mwinyi Zahera kitashuka dimbani leo kikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri baada ya kurejea kikosini kwa wachezaji wake waandamizi waliolkuwa majeruhi nahodha Kelvin Yondani, Gadiel Michael na Papi Tshishimbi
Hata hivyo Yanga itawakosa Ibrahim Ajib na Mrisho Ngasa wanaotumikia adhabu ya kadi wakati kinara wa mabao Heritier Makambo ana uwezekano mdogo wa kucheza baada ya kuumia mazoezini
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa leo kuwaunga mkono mabingwa hao wa kihistoria
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A - 15,000/-
VIP B na C - 10,000/-
Mzunguuko - 5,000/-

ADVERTISE HERE