Simba yapania kusajili kisasa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Apr 2019
Simba yapania kusajili kisasa

Wajumbe wa Bodi ya Simba wamependekeza sera mpya ya usajili ambayo huenda ikatumika kuanzia mwezi ujao kushusha wachezaji wapya katika kikosi cha Simba

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema sera hiyo wameikopi kutoka barani Ulaya na wanaamini itakuwa na manufaa kwa klabu hiyo inayojiendesha kisasa

Magori amesema sera hiyo mpya itapitishwa na wajumbe na itatumika kufanya usajili wa wachezaji wapya wa msimu ujao.

Sera hiyo itakuwa na mambo sita ambapo amefafanua baadhi

Jambo la kwanza katika sera mpya ya usajili itaangalia kama aina ya usajili inafanana na malengo ya timu, baada ya hapo itaangaliaa bajeti ya klabu katika usajili ni kiasi gani na aina ya wachezaji ambao wanaweza kupatikana kulingana na bajeti

"Tumefuatilia usajili wa klabu nyingine Afrika na kuona ni lazima uongozi utenge bajeti ya usajili ambayo inakuwa wazi kila mtu anaifahamu na hata usajili ambao unafanywa unalingana na kiasi cha pesa ambacho klabu inacho," Magori amenukuliwa na Mwanaspoti

"Suala jingine lipo katika sera hiyo mpya msimu huu tutaangalia upungufu uliojitokeza msimu uliopita unaendana na usajili wa wachezaji wapya ambao tunataka kuufanya? Hii ni kwa sababu hatutakuwa tena na usajili ule wa kugombania mchezaji"

Magori alifunguka zaidi kuwa sera itaangalia usajili wa mchezaji mpya ana umri gani na nafasi yake ambayo anacheza na umri aliokuwa nao vinaendana na kama atakuwa na umri mzuri kulingana na nafasi ambayo inatakiwa kuongezwa nguvu

Pia sera hiyo inataka kila kwenye usajili ambao timu itakuwa inafanya lazima kuwa mtu mwenye sauti ya mwisho mwenye kuamua mchezaji mpya wa kusajiliwa kulingana na nafasi ambayo tunahitaji na vile vigezo ambavyo vimewekwa.

"Hapa kwenye maamuzi ya mwisho ndiyo tunaweza kuongezeka nafasi nyingine kwani Bodi ya Wakurugenzi ndiyo itakuwa na maamuzi ya mwisho kulingana na ripoti ya mwalimu kulingana na wachezaji wapya ambao atakuwa anawahitaji"

"Sera hiyo mpya inaonesha pia kama si Bodi ya Wakurugenzi basi benchi la ufundi linaweza kuwa na maamuzi na kauli ya mwisho katika usajili bila kuingiliwa kama alivyokuwa akifanya Arsene Wenger pale Arsenal, vilevile sera itatuwezesha kuchagua njia ya viongozi ndio kuwa wenye kauli ya mwisho"

"Jambo la mwisho sera mpya inaonesha tunaweza kuunda kamati maalumu ambayo watachanganyika watu mbalimbali kufanya usajili ambao wao ndio watakuwa wenye kauli ya mwisho baada ya kocha kutoa mapendekezo yake, au tunaweza kuunda kamati maalumu iliyokuwa na makocha wazoefu nchi na nje ya nchi akiwepo na kocha wetu hao ndio watakuwa kila kitu katika usajili"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’