Dewji aitabiria Simba nusu fainali ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Apr 2019
Dewji aitabiria Simba nusu fainali ligi ya mabingwa

Mfanyabiashara maarufu nchini aliyewahi kuifadhili timu ya soka ya Simba kwa mafanikio makubwa, Azim Dewji ameitabiria makubwa klabu hiyo katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwishoni mwa wiki hii huko mjini Lumbumbashi.

Dewji amesema Simba ya mwaka huu ni `moto’ na ina uwezo wa kuwang’oa Mazembe kutokana na kuundwa na wachezaji wenye vipaji na ari ya kupata matokeo chanya.

Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Dewji aliyeifikisha Simba fainali za Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 1993, alisema kitu pekee kinachopaswa kufanywa na wachezaji na viongozi wa Simba ni kuondoa mchecheto wa mchezo na badala yake kuelekeza nguvu katika mchezo wa marudiano

"Ni kweli Mazembe ni timu ngumu na kongwe. Ukiangalia ina historia kubwa Afrika na ndani ya miaka hii kumi tumeshuhudia ikitwaa ubingwa tofauti wa michuano ya CAF mara tano.  Ni rekodi bora sana, lakini pamoja na ubora wao, nikiangalia ubora na uthubutu wa wachezaji wa Simba, naona vijana wetu wanaweza kufanya kweli," Dewji amenukuliwa na Bin Zubeiry

"Wachezaji wa sasa wa Simba nawafananisha na wale wa enzi zile tunafika fainali CAF.

"Walikuwa wanajituma sana uwanjani. Na hawa ukiwaangalia wana kila kitu kinachoweza kuwaduwaza Mazembe kwao.

"Angalia walivyowakimbiza hapa Dar es Salaam, kwa kawaida Mazembe si wa kujiangusha hivyo, lakini uliona katika mchezo wa kwanza, walizidiwa sana ila bahati haikuwa kwa Simba.

"Na hata hao wanaobeza penalti ya John Bocco watambue Simba hii ni moto wa kuotea mbali na usishangae kuona mpira umetangulia Lubumbushi na wachezaji wanakwenda kumalizia kazi ya kuandika historia zaidi kwa soka ya Tanzania," alisema

Akizungumzia tukio la klabu hiyo kupinga kubadilishiwa mwamuzi wa mchezo wa marudiano dhidi ya Mazembe, alisema jambo hilo litawarejesha mchezoni wachezaji, lakini pia kuongeza umakini wa waamuzi katika mchezo huo.

"Hata kama CAF hawatabadilisha uamuzi huo, mwamuzi aliyepangwa (Janny Sikazwe wa Zambia) atakuwa makini zaidi na kizuri ni kwamba hatataka kuharibu sifa zake zilizomwezesha kuchezesha michuano karibu yote mikubwa duniani.

"Amechezesha Kombe la Dunia mara mbili, Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, pia fainali za Klabu Bingwa ya Dunia, achilia mbali hii michuano ya klabu Afrika," alisema Dewji aliyewataka Watanzania kuendelea kuwaunga mkono wawakilishi hao wa taifa.

Katika mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, timu hizo hazikufungana, hivyo kuzifanya timu zote kuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali, matokeo ya mwishoni mwa wiki yakiwa mwamuzi wa mwisho.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’