Mkakati wa kuimaliza TP Mazembe waanza mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Mar 2019
Mkakati wa kuimaliza TP Mazembe waanza mapema

Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi jana kwenye uwanja wa Boko Veterans ikiwa ni maandalizi ya viporo vya ligi kuu na mchezo muhimu wa robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazembe

Kuelekea mchezo huo dhidi ya TP Mazembe, Simba inaandaa mkakati wa kuhakikisha inapata matokeo ya kuipeleka hatua ya nusu fainali

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema wanahitaji kufanya vizuri katika mchezo huo

Amesema viongozi watakutana kupanga mkakati wa kuhakikisha wanaivusha Simba kwenda hatua ya nusu fainali

"Kupitia kikao hicho, tutapanga mkakati wetu ingawa timu tayari ilianza maandalizi yake tangu hatua ya awali mpaka hapa tulipofikia," amesema Magori

"Niwahakikishie Wanasimba wote kwamba sisi viongozi hatulali na badala yake tunafanya kila linalowezekana kushinda, hata sasa tulisubiri mchezo wa Stars dhidi ya Uganda umalizike, tukutane tena," alisema Magori.

Simba imepata ushindi katika michezo yake yote ya ligi ya mabingwa iliyopigwa katika dimba la Taifa kwenye hatua ya makundi lakini ikapoteza ya ugenini kwa kufungwa jumla ya mabao 12

Magori amesema watahakikisha hawarudii makosa ya kufungwa mabao mengi ugenini huku akitilia mkazo ushindi kwenye mchezo wa kwanza utakaopigwa uwanja wa Taifa April 05 2019

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
4h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
5h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
7h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’