Mo aiombea dua Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Mar 2019
Mo aiombea dua Stars

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewahamasisha wachezaji wa Taifa Stars kuipigania Tanzania Jumapili, wawaze kushinda mchezo dhidi ya Uganda Cranes

Mo amesema Watanzania wote tunapaswa kuwa wamoja kuelekea mchezo huo ambao Stars inahitaji kushinda ili iweze kukata tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Misri baada ya kukosa michuano hiyo kwa miaka 39

Mo amewahakikishia wachezaji wa Stars kuwa Watanzania wote wako nao kwani wanashauku ya kuiona timu yao ikifuzu kwa fainali za michuano hiyo, hivyo wasiwaangushe

"Watanzania wote tupo nyuma yenu wachezaji wetu wa Taifa Stars kuhakikisha tunashinda dhidi ya Uganda, sababu zote za kufanya hivyo tunazo," amesema

"Naamini mtashinda na kutufanya Watanzania tutembee kifua mbele. Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu mfanye"

Kuelekea mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Jumapili saa 12 jioni katika dimba la Taifa, mashabiki wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuwapa sapoti wachezaji

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ambao kiingilio ni Tsh 2000/- tu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’