Beki Kelvin Yondani na kiraka Erasto Nyoni leo wamewakosha mashabiki wa soka nchini baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mchezo dhidi ya Cape Verde.
Yondani hakucheza katika mchezo uliopigwa kule Cape Verde wakati Nyoni yeye hakuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichosafiri visiwani humo.
Lakini baada ya mashabiki kupaza sauti juu ya umuhimu wa wakongwe hao, Kocha Amunike alisikia kilio cha wengi na hakika mwenyewe amejionea 'shughuli' ya wakali hawa dimbani.
Yondani aliwamudu ipasavyo washambuliaji wa Cape Verde wakati Nyoni shughuli aliyokuwa anaifanya katikati ya dimba ilikuwa sio ya nchi hii..!
Kwa ujumla wachezaji wote wa Stars wanastahili pongezi kwa juhudi zao walizoonyesha kwenye mchezo wa leo.
Kikosi hiki kinaweza kufuzu kwa fainali za AFCON 2019.

ADVERTISE HERE