Samatta aipongeza Simba, aiombea ushindi dhidi ya TP Mazembe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Mar 2019
Samatta aipongeza Simba, aiombea ushindi dhidi ya TP Mazembe

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Simba imepangwa kuchuana na TP Mazembe katika mchezo wa robo fainali

Samatta ambaye kwa sasa ni kinara wa upachikaji mabao ligi kuu ya Ubelgiji akiwa na klabu ya KRC Genk, amewahi kuzitumikia Simba na TP Mazembe

Samatta aliitumikia Simba kwa muda mfupi kabla ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kumuuza TP Mazembe ambako aliweza kupata mafanikio zaidi

Akiwa na TP Mazembe, mwaka 2015 aliweza kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la ligi ya mabingwa Afrika yeye akiibuka kuwa mfungaji bora akipachika mabao saba

Mafanikio hayo yalimpa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani

Samatta amesema kwa hatua waliyofikia Simba, wanaweza kusonga mbele zaidi kwani wanaouwezo sawa na timu nyingine wanazoshindana nazo

Licha ya kucheza TP Mazembe kwa muda mrefu, Samatta amesema angependa kuona Simba inapata ushindi katika mchezo baina ya timu hizo ili iweze kutinga nusu fainali

"Simba sio wabaya, ukiangalia wote walioingia nao katika hatua ya robo fainali, kinachowatofautisha ni uzoefu wa kucheza mashindano ya Afrika," amesema Samatta

"Kinachotakiwa ni maandalizi mazuri na nina imani wanao uwezo wa kufika mbali kwa sababu hata hapa walipofikia ni jitihada walizofanya katika maandalizi"

"Kama Mtanzania ningependa kuona Simba inafika mbali zaidi katika michuano hii"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’