Ibenge aivulia kofia Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Mar 2019
Ibenge aivulia kofia Simba

Kocha Mkuu wa AS Vita Club Florent Ibenge amesema Simba ilistahili kushinda mchezo wa jana kutokana na kuwa katika kiwango bora kuliko timu yake

Vita Club ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba na kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikiiacha Simba ikitinga robo fainali

Akizungumza baada ya mchezo jana, Ibenge alisema Simba ina wachezaji wazuri

Aidha, Ibenge alifichua kuwa walimuwekea ulinzi mkali Meddie Kagere kwa kuwa ndio mchezaji waliokuwa wakimuhofia zaidi

"Simba walionyesha ushindani mkali kwetu, walicheza vizuri matokeo waliyopata walistahili, tunawapongeza," amesema

"Kagere ndio mchezaji tuliyekuwa tunamuhofia zaidi na niliwaagiza wachezaji wangu wamchunge lakini mwisho wa siku mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa tumeadhibiwa"

Mabao ya Simba yalifungwa na Mohammed Hussein na Clatous Chama aliyefunga bao la ushindi katika dakika za lala salama

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’