Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wamesema wako tayari kuikabili Cape Verde kesho kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.
Winga machachari anayechezea Difaa Al Jadida Saimon Msuva amesema kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo wa kesho.
"Hali ni nzuri na morali ipo juu, kila mtu anajua umuhimu wa hii mechi na kila mchezaji ukimuuliza anafahamu umuhimu wake.
"Tuna mechi mbili tunaanza hapa (Cape Verde) halafu tutarudiana nyumbani. Tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho."
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa Jumanne, Oktoba 16 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Matokeo ya ushindi au sare kwa Stars kwenye mchezo wa kesho yataiweka katika nafasi nzuri hasa kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo wa nyumbani Jumanne.

ADVERTISE HERE