Kulekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika, Afisa Habari wa Simba Haji Manara leo anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuweka wazi mikakati ya ushindi
Mkutano huo utafanyika Makao Makuu ya klabu ya Simba yaliyoko mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam
Wakati huo huo kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka leo nchini Algeria kurejea nchini tayari kwa mchezo huo dhidi ya AS Vita Club utakaopigwa Jumamosi, March 16 katika dimba la Taifa, saa moja usiku
ADVERTISE HERE