Kocha Msaidizi wa Simba Denis Kitambi amesema wamedhamiria kupata matokeo mazuri kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura na kuondoa 'nuksi' ya kufanya vibaya kwa michezo ya ugenini katika michuano ya ligi ya mabingwa
Akizungumzia maandalizi ya kikosi cha Simba, Kitambi amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo unaopigwa ugenini
"Ni lazima tupate matokeo nyumbani na ugenini. Nafahamu itakuwa changamoto kuifunga JS Saoura kwenye uwanja wao hasa ikingatia tuliwafunga tulipocheza nao jijini Dar es salaam lakini hatupaswi kukata tamaa," amesema
"Ni lazima tupambane, tujitume kwa jitihada zote ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri"
"Tutajiimarisha kimbinu zaidi kwani tunafahamu ni lazima tubadilike kwenda sambamba na ukubwa wa mashindano. Hatuwezi kucheza sawa na tunavyocheza katika ligi kuu"
Kikosi cha Simba leo kimeendelea na mazoezi nchini Algeria kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki