Kakolanya aeleza mafanikio yake mchezo dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2018
Kakolanya aeleza mafanikio yake mchezo dhidi ya Simba
Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya juzi aliibuka nyota wa mchezo wa pambano la watani wa jadi baada ya kufanikiwa kuzuia mashambulizi mengi langoni na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Kakolanya amesema siri kubwa ya mafanikio yake kwenye mchezo huo ni kuwa na utulivu langoni.

Amesema alijitahidi kufanya maamuzi sahihi kila alipotokea mipira lakini pia ushirikiano na wachezaji wenzake wa Yanga ulisaidia kwa kiasi kikubwa kufanya wapate matokeo hayo.

"Nilibaini washambuliaji wa Simba walikuwa wana kasi hivyo nami nikawa nafanya uamuzi wa haraka kila nilipotokea mpira."

"Kwa kweli haikuwa rahisi lakini kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu tulipata matokeo yake na kuweza kuondoka na alama moja ambayo sio mbaya kwetu."

Kakolanya pia amesema baada ya mchezo huo alipokea pongezi nyingi kutoka kwa wachezaji wenzake, viongozi, wanachama na mashabiki wa Yanga.

Kakolanya alituzwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na WanaYanga kutokana na kazi kubwa aliyofanya kwenye mchezo huo.

Kiwango alichoonyesha juzi huenda kikampa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha timu ya Taifa mbele na kipa wa Simba Aishi Manula ambaye kwa sasa ni chaguo la kwanza kwenye kikosi hicho.

Stars tayari imeingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya kutinga fainali ya michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’