Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinaondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc utakaopigwa Jumanne, Februari 26 katika dimba la Samora
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timju inaondoka leo jijini Dar es salaam na kikosi cha wachezaji 26 ambapo itaweka kambi ya siku moja mkoani Morogoro
Leo jioni Simba inatarajiwa kufanya mazoezi Morogoro kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Iringa hapo kesho
"Tunaondoka leo na kikosi cha wachezaji 26. Ni mchezaji mmoja tu, Shomari Kapombe ambaye hatasafiri na timu. Erasto Nyoni amejumuishwa katika kikosi hicho," amesema Rweyemamu
Rweyemamu aliongeza kuwa hali ya mshambuliaji Emmanuel Okwi inaendelea vizuri na amejumuishwa katika kikosi kinachosafiri leo
"Hali ya Okwi inaendelea vizuri, alipata majeraha ya kuchanika chini ya jicho kwenye mchezo wa jana dhidi ya Azam Fc. Ameshonwa nyuzi mbili na hali yake inaendelea vizuri"