Ushirikiano utatupa mafanikio msimu huu - Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2018
Ushirikiano utatupa mafanikio msimu huu - Abdul
Nahodha Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema ni mapema kuweka wazi silaha zake kwa wapinzani ila anachokiamini Yanga inanafasi kubwa ya kufanya vizuri katika ligi kutokana na ukaribu wa viongozi kwa wachezaji wao.

Abdul alisema alikuwa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha, lakini anamshukuru Mungu amerudi katika majukumu yake na kuweka wazi kuwa anatarajia kuonyesha jitihada zaidi katika mazoezi ili kocha aweze kupewa nafasi ya kurudi haraka uwanjani.

"Nimeshaanza mazoezi na naendelea vizuri na mazoezi nafasi ya kucheza katika mchezo unaofuata namuachia mwalimu kwani yeye ndiye anayejua nani ni muhimu kikosini kwa wakati gani, lakini kwa upande wangu nipo tayari kwaajili ya mapambano," alisema beki huyo.

Akizungumzia ligi kwa ujumla alisema ligi ni ngumu kila timu inaonyesha imejipanga kwaajili ya ushindani ili kujitengenezea mazingira mazuri katika msimamo na ligi kwa ujumla.

Abdul alisema wao kama wachezaji wamekaa na kukubaliana kuwa ni muhimu sana wakatumia vizuri michezo yao yote ya uwanja wa nyumbani kwa lengo la kuhakikisha wanajitengenezea mazingira mazuri ya kuhakikisha wanajiweka katika nafasi nzuri ya kurudisha ubingwa waliokuwa wanaishukilia na kunyang'anywa na Simba.

"Nawapongeza wachezaji wenzangu kwa pointi tisa walizozipata katika michezo mitatu tuliyocheza naamini bado tutaendelea kuvuna pointi zaidi katika michezo yetu, tunatarajia kukutana na Singida ambao wamekuwa wagumu sana kwetu lakini msimu huu wasitegemee pointi tatu kwetu tumejipanga na tutawafunga.

"Singida United tunawaheshimu ni wazuri, lakini sisi ni wazuri zaidi yao hilo litaonekana baada ya dakika tisini lakini kiujumla kikosi chetu ni bora na kinaendelea vizuri kikiwa chini ya kocha Mwinyi Zahera ambaye anaonekana anatamani timu yetu ipate mafanikio kutokana na kuwa na mbinu nyingi ambazo zimekuwa na chachu ya mafanikio," alisema Abdul.

Kuelekea mpambano wa watani wa jadi, Abdul alisema Simba ni timu kama zilivyotimu nyingine walizokutana nazo na kupata matokeo hivyo hata wao watawafunga tu na kila mmoja atashangaa kutokana na kile kitakachotokea siku hiyo.

"Ni mapema sana kuizungumzia Simba, lakini kikubwa ninachoweza kukisema ni kwamba hata wao watafungwa kwa sababu ni miongoni mwa timu zitakazochezwa Dar es Salaam na mipango yetu ni kupata pointi zote za uwanja wa nyumbani hivyo muda ndio utakaoongea sasa tunaitazama zaidi Singida United," alisema.

"Unajua mchezo wa Simba na Yanga ndio unaotazamwa na mashabiki na kujikuta wanasahau kabisa kama kuna michezo mingine muhimu pia na inasaidia timu kujitengenezea mazingira ya kutwaa ubingwa naomba niwaombe mashabiki wetu kuangalia kwa ukaribu na michezo mingine waachane na suala la Usimba na Uyanga," alisema Abdul.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’