Kagere mbabe wa mechi muhimu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Feb 2019
Kagere mbabe wa mechi muhimu

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere msimu wake wa kwanza umekuwa na mafanikio mpaka sasa akiongoza kwa kupachika mabao katika michuano yote

Kagere ameifungia Simba mabao 11 kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara, jana akifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Azam Fc

Katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kagere anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya vinara wa ufungaji akiwa amefunga mabao manne kuanzia raundi ya kwanza ya michuano hiyo

Lakini jambo kubwa analolifanya Kagere ambalo linainufaisha sana Simba ni mabao yake anayofunga kwenye michezo muhimu

Katika kipindi cha mwezi mmoja Kagere amefungia Simba mabao sita kwenye michezo muhimu

Aliifungia Simba mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura, akafunga bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Al Ahly na akarudia tena dhidi ya Yanga.

Jana akafunga tena mabao mawili kuipa Simba ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Azam Fc

Simba haikukosea kumsajili mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Rwanda aliyekuwa akiitumikia Gor Mahia ya nchini Kenya

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’