Zahera apigia hesabu pointi tatu za Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2018
Zahera apigia hesabu pointi tatu za Singida United
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema mipango na mazoezi yake yote sasa ni kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mazoezi jana, Zahera, alisema kwa sasa wamesahau matokeo ya mchezo uliopita na amewataka wachezaji wake kuelekeza akili na nguvu katika mechi ya kesho.

Zahera ambaye alitua Yanga akirithi mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, alisema anawaandaa wachezaji wake kulingana na aina ya mpinzani, lakini akiwakumbusha kuwa mechi zote ni muhimu na anahitaji kuondoka na pointi tatu muhimu.

β€œKwangu kila baada ya kumalizika mchezo mmoja wa ligi, naanza kufikiria mchezo unaofuata, mipango na mikakati ya sasa ni mchezo ujao dhidi ya Singida United,” alisema Zahera.

Aliongeza kuwa katika kuongeza nguvu katika kikosi hicho, tayari amewarejesha nyota wake ambao aliwasimamisha na kutokuwa sehemu ya wachezaji walioivaa Coastal Union ya Tanga.

β€œKila kitu kipo sawa kwa sasa, muhimu nataka kila mchezaji wangu azingatie nidhamu ndani na nje ya uwanja, hatuwezi kuwa na umoja na hali ya ushindi kama hakutakuwa na nidhamu,” alisema Zahera ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Alisema kuwa bado kuna makosa madogo ambayo aliyaona katika mchezo dhidi ya Coastal Union licha ya kupata ushindi bao 1-0, ameyafanyia kazi ili yasijirudie.

"Sasa hivi tunajipanga kwa mchezo unaofuata, lakini kila baada ya mchezo nafanyia kazi mapungufu au kasoro ninazoziona, yapo makosa madogo niliyoyaona kwenye mchezo uliopita, nimeshayafanyia kazi, nataka kuona tunapata ushindi katika kila mchezo,” aliongeza kocha huyo.

Yanga ina pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote tatu ilizocheza katika ligi hiyo ambayo kinara wake ni Mbao FC ya jijini Mwanza yenye alama 10 baada ya kucheza michezo mitano.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’