Baada ya kuiangamiza Yanga juzi, mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amesema ataendelea kutimiza wajibu kwa kuisaidia yake kushinda kila mchezo
Juzi Kagere alifikisha mabao tisa, akihitaji kufunga mabao mawili zaidi ili kumfikia Heritier Makambo wa Yanga anayeongoa orodha ya wafungaji bora msimu huu akiwa na mabao 11
Kagere, mshambuliaji wa Kimataifa raia wa Rwanda amekuwa katika kiwango bora akiifungia Simba mabao muhimu kwenye ligi na michuano ya ligi ya mabingwa
"Kazi yangu mimi ni kufunga. Nitaendelea kufanya hivyo kila nitakapopewa nafasi ya Mwalimu ili kuisaidia timu yangu ipate ushindi," alisema Kagere jana akiwa na kikosi cha Simba mkoani Arusha
Kesho Jumanne Kagere ataiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon