Bodi ya ligi kuziba pengo la Sanga Novemba 17

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Sep 2018
Bodi ya ligi kuziba pengo la Sanga Novemba 17
Uchaguzi mdogo wa Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara wa kujaza nafasi zilizo wazi utafanyika Jumamosi Novemba 17, mwaka huu mjini Dar es Salaam.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba Fomu kwa ajili ya wagombea zitaanza kutolewa Septemba 21, mwaka huu kwenye ofisi za shirikisho hilo.

"Muda wa mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ni Saa 10:00 jioni Septemba 25, 2018,"amesema Ndimbo.

Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Kuu (PL), Mjumbe mmoja kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha Klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL).

Ada ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti ni Sh. 200,000 (Shilingi laki mbili) wakati nafasi nyingine zilizobaki ni sh.100,000 (Shilingi laki moja).

Uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

Wagombea kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ni marais au Wenyeviti wa Klabu husika, Hivyo, Wagombea wanatakiwa kuwa Wenyeviti au Marais wa Klabu husika.

Nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB inagombewa na Klabu za Ligi Kuu pekee. Ikumbukwe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Clement Sanga alipoteza sifa baada ya klabu ya Yanga kumrejesha Mwenyekiti wake Yusufu Manji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’