Kocha Yanga akiri 'mziki' wa Simba sio saizi yake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Feb 2019
Kocha Yanga akiri 'mziki' wa Simba sio saizi yake

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ubora wa kikosi cha Simba ndio sababu iliyopelekea timu yake kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa leo

Zahera aliyekuwa akizungumza sana kuelekea mchezo huo, amelazimika kukiri kuwa ubora wa Simba kwa sasa hauwezi kulinganisha na timu yake

"Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia waandishi wa habari kuwa Simba wana timu nzuri. Tumepoteza mchezo wa leo kwa sababu hiyo," amesema Zahera

Naye Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema waliingia katika mchezo huo wakiwa na malengo ya kuibuka na ushindi, amefurahishwa na matokeo hayo

"Lengo letu ilikuwa ni kupata alama tatu sababu ulikuwa mchezo muhimu, tulicheza vizuri na kiukweli tulistahili kushinda. Muhimu tumepata ushindi na kwakweli nimefurahi," amesema Aussems

Ushindi wa leo umeendelea kudhihirisha umwamba wa Simba dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi.

Yanga haijaonya radha ya ushindi dhidi ya Simba kwa msimu wa tatu mfululizo sasa

Mara ya mwisho Yanga kuifunga Simba ilikuwa msimu wa 2015/16 wakati huo ikinolewa na Hans van Pluijm ambaye kwa sasa ni kocha wa Azam Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’