Rage ataka kipigo cha 'mbwa koko' kwa Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Feb 2019
Rage ataka kipigo cha 'mbwa koko' kwa Yanga

Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage amesema haoni kama Yanga itaweza kunusurika na kipigo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara keshokutwa

Rage amesema anaamini ushindi wa bao 1-0 iliyopata Simba dhidi ya Al Ahly juzi umeongeza 'moto' kuelekea mchezo huo

"Ili Yanga watuheshimu tunatakiwa kuwafunga mabao 6-0 heshima itakuwepo wanatakiwa kutambua kuwa sisi tuna timu bora na ndio timu pekee ambayo inaiwakilisha nchi vizuri katika mashindano ya Klabu Bingwa," amesema.

"Wachezaji wa Simba wanapaswa kuacha kulewa sifa za ushindi walioupata na kuwadharau Yanga, waendelee na maandalizi mazuri."

Kikosi cha Simba chini ya kocha Mkuu Patrick Aussems ambaye sasa atasaidiwa na Denis Kitambi kimejichimbia jijini Dar es salaam kikiendelea na maandalizi ya mchezo huo

Tangu kutua kwa Aussems, Simba imeachana na utaratibu wa kuweka kambi nje ya jiji la Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’