Yanga haikujipangia ratiba yake - Ten

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
Yanga haikujipangia ratiba yake - Ten
Baada ya kuwapo na maneno kuwa Yanga imependelewa kwa kupangwa kucheza mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, uongozi umeibuka na kusema kuwa wao hawakuomba.

Akizungumza jana jijini, Msemaji wa Yanga, Dismas Ten, alisema kuwa ratiba hiyo imepangwa na Bodi ya Ligi na klabu yake imeipokea kama ilivyotolewa.

β€œSiwezi kuzungumzia timu nyingine, lakini hii ratiba inayosemwa imepangwa na bodi ya ligi, sisi tunaifuata tu,” alisema Ten.

Katika mechi hizo 11 ambazo itacheza hapa jijini, michezo saba klabu hiyo inayofundishwa na Mwinyi Zahera itakuwa nyumbani na iliyobakia watakuwa ugenini.

Simba inayotoa malalamiko hayo pia itakuwa na michezo nane mfululizo uwanja wa Taifa baada ya kumaliza michezo yao mitatu ya mikoani.

Kwa sasa Yanga yenye pointi tatu na iliyoshuka dimbani mara moja inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi dhidi ya Stand United kutoka Shinyanga ambayo itafanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

Ligi hiyo inayotoa mwakilishi wa Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajia kuendelea tena leo kwa Mwadui FC kuwakaribisha mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam FC wakati African Lyon itawaalika Coastal Union ya jijini Tanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’