Jina lake lilipoonekana kwenye kikosi kinachoanza mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly baadhi ya mashabiki walikosa imani kwake
Lakini ukizungumzia wachezaji wlaiofanya vizuri katika mchezo wa leo, hutakuwa umemtendea haki Zana Coulibaly kama hutataja jina lake
Goli la Simba lililofungwa na Meddie Kagere lilianzia mguu kwake kwani krosi yake ndio iliyozaa bao hilo
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliwahi kusema, Zana ni mchezaji mzuri kwa sasa wengi wanaweza wasiamini lakini anahitaji muda kuyazoea mazingira mapya
Wakati mwingine ni vyema kuyaamini maamuzi ya makocha kwani wao wana ufahamu zaidi kuliko mashabiki
ADVERTISE HERE