Simba dimbani leo kuikabili Mwadui Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Feb 2019
Simba dimbani leo kuikabili Mwadui Fc

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo Alhamisi watashuka katika dimba la Taifa kuikabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 25

Baada ya kubanwa na majukumu ya Kimataifa kwa wiki kadhaa, Simba leo saa moja jioni inarejea uwanjani kuwapa furaha mashabiki wake

Mchezo huo pia utakuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Simba ambacho Jumanne ijayo kitaikabili Ah Ahly katika mchezo wa ligi ya mabingwa

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika.

Ukiondoa wachezaji majeruhi wa muda mrefu, wengine wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo

Simba inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 33.

Hata hivyo ina michezo 10 pungufu ya KMC na Lipuli zinazoshika nafasi ya nne na tatu, michezo saba pungufu ya Azam na nane pungufu ya Yanga inayoongoza ligi ikiwa na alama 55

Kimahesabu, Simba itaweza kuongoza ligi kama itashinda michezo yake yote ya viporo

Simba imedhamiria kutetea ubingwa wake, ushindi ndio matokeo ambayo Wana Msimbazi wanahitaji leo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’