Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mabingwa hao wa Tanzania Bara bado wana nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kama watatumia vyema michezo miwili iliyobaki nyumbani
Aussems amesema hakuna sababu ya kukatishwa tamaa na vipigo vya mabao 5-0 iliyofungwa Simba dhidi ya Vita Club na Al Ahly, muhimu ni kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi Jumanne ijayo kuiunga mkoni Simba itakapokuwa ikirudiana na Al Ahly
"Hatuwezi kukatishwa tamaa na michezo miwili iliyopita kwani bado tuna michezo miwili ya nyumbani ambayo tunaweza kufanya vizuri," amesema Aussems
"Ni muhimu kwa mashabiki wetu kuendelea kuishangilia timu na kujitokeza kwa wingi katika mchezo ujao wa siku ya Jumanne ambao tutacheza na Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam"
Simba bado ina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo kama itafanikiwa kushinda michezo miwili ya nyumbani