Baada ya kufuta mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United uliokuwa upigwe leo mkoani Kigoma, Jumapili ijayo, Septemba 09 Yanga itajipima na African Lyon kwenye uwanja wa Uhuru.
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema mchezo huo watautumia kukiweka kikosi chao kwenye ushindani wakati huu ambao ligi imesimama kwa karibu wiki mbili kupisha michuano ya Kimataifa iliyo kwenye kalenda ya FIFA.
Yanga imeendelea kujifua kwenye uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa kwa ajili ya michezo ya ligi.

ADVERTISE HERE