Klabu ya Pharco Fc ya nchini Misri imefika dau kumsajili kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya.
Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa katika mazungzo ya mwisho na Pharco Fc inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri
"Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya nchini Misri kuhusu mchezaji Shiza Kichuya kwenda kujiunga na timu hiyo. Taarifa zaidi itatolewa baadae baada ya taratibu zote kukamilika," imesema taarifa ya Simba
Kichuya yuko kwenye kikosi cha Simba ambacho tayari kiko nchini Misri kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa Jumamosi, Februari 02 2019
ADVERTISE HERE