Chama cha Soka nchini Misri (EFA) kimesema kuwa klabu ya Al Ahly imepewa kibali cha kuingiza uwanjani mashabiki 10,000 tu katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi Februari 02 2019
Baada ya klabu ya Ismailia kuondoshwa katika michuano hiyo kutokana na vurugu za mashabiki, Jeshi la Polisi la Misri limechukua hatua ya kudhibiti idadi ya mashabiki wanaoingia uwanjani
Timu hiyo inatarajiwa kuanza kuuza tiketi za mchezo huo leo
Al Ahly ndio vinara wa kundi D wakiwa na alama nne wakifuatiwa na Vita Club yenye alama tatu sawa na Simba timu hizo zikitofautina mabao tu
Katika mchezo huo Al Ahly haitakuwa na kiungo wake tegemeo Walid Soliman anayetarajiwa kuwa nje kwa wiki tano kutokana na majeraha lakini wachezaji wake watatu, beki Saad Samir, mshambuliaji Sala Mohsen na winga Geraldo wamerejea kikosini baada ya kupona majeraha yao
Tayari Simba imetua nchini Misri na itaanza kujifua leo kujiweka sawa na hali ya baridi kali la nchi hiyo