Jana baada ya mchezo dhidi ya Rayon Sports, kiungo wa Simba Haruna Niyonzima alifika katika Hotel waliyokuwa wameweka kambi Yanga kuwasalimu wachezaji wenzake.
Licha ya kuwa ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda, Niyonzima yuko nchini humo kwa karibu miezi miwili sasa baada ya kutofautiana na uongozi wa klabu ya Simba.
Kuna taarifa mchezaji huyo huenda akavunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki kama watashindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Simba.
Niyonzima ameitumikia Yanga kwa muda mrefu, haishangazi kuendelea kuwa na ukaribu na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara.
Hivi karibuni alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akisema kuwa angependa kurudi kucheza Yanga siku moja.

ADVERTISE HERE