Mo hataki masihara, achukua hatua 'fasta' baada ya kipigo cha Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2019
Mo hataki masihara, achukua hatua 'fasta' baada ya kipigo cha Vita

Ni faraja kuona mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' kwa kushirikiana na uongozi wa klabu hiyo mara moja wamechukua hatua ya kukiimarisha kikosi kinachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mchezo dhidi ya AS Vita Club umetoa taswira ya ugumu wa michuano hiyo hasa kwa michezo ya ugenini.

Ili Simba iweze kufuzu hatua ya robo fainali na pengine kuwaza kutwaa ubingwa kuna ulazima wa kuboresha kikosi chake

Jana Simba imeshusha wachezaji wawili kutoka nchi za Ghana na Togo huku ikielezwa mchezaji mwingine kutoka Namibia yuko njiani

Wachezaji hao ni beki wa kati, Mghana Moro Lamine na straika Mtogo Hunlede Kissimbo Ayi na walianza kufanya mazoezi na Simba jana Jumatatu jioni katika Uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam

Kama watafuzu majaribio, wawili hao wanaweza kuongezwa katika kikosi kinachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa mwaka huu

Kwa mapungufu yaliyoonekana katika mchezo dhidi ya Vita, hakuna ubishi kuwa Simba inahitaji kuboresha safu yake ya ulinzi pamoja na kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji

Ikumbukwe pia bado hatma ya mshambuliaji wake tegemeo Emmanuel Okwi anayewaniwa na Kaizer Chiefs bado haijafahamika

Okwi huenda akaondoka mwishoni mwa msimu mkataba wake utakapomalizika hivyo ni vyema kwa Simba kusaka mbadala wake mapema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’