Wimbo wa Yanga uko tayari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2018
Wimbo wa Yanga uko tayari
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema ule wimbo maalum wa klabu ya Yanga tayari umekamilika na huenda ukaanza kusikika leo uwanja wa Taifa kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ten amesema wimbo huo uliotengenezwa na Lamar (Fishcrab Record) utafanyiwa mazoezi kwa aina tofauti za uimbaji na ushangiliaji.

"Lamar amethibitisha kuwa ule wimbo maalum wa klabu yetu uko tayari.

"Usikose Uwanja wa Taifa leo tuje kufanya mzoezi kabla haijatoka rasmi kwa style mbalimbali za kushangilia ambazo tutazitumia wakati wa kurekodi video na wakati wote ambao tutakuwa tukiimba jukwaani pamoja wakati Yanga iko uwanjani 'inakinukisha'," ameandika Ten kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuwa na wimbo wake maalum wa kuitambulisha klabu ambao utatumiwa na mashabiki kwa ajili ya kuhamasisha.

Katika ligi mbalimbali barani Ulaya hasa Uingereza, Hispania na Ujerumani tumeshuhudia timu nyingi zikiwa na nyimbo zao ambazo huimbwa na mashabikui muda wote kabla na wakati wa mchezo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’